Kutoka Kibera matopeni hadi kwa Prado TX, Manzi wa Kibera adai kununua gari

Muhtasari

• Manzi wa Kibera amewashangaza wengi baada ya kupakia video za kushawishi mitandaoni kwamba hatimaye amekuwa mmoja kati ya wamiliki wa gari la kifahari aina ya Prado TX.

Manzi wa Kibera na gari analodai kuwa lake
Manzi wa Kibera na gari analodai kuwa lake
Image: Instagram Screenshot

Miezi kadhaa baada ya kudai kwamba anaishi katika hali ya umaskini mkubwa licha ya umaarufu uliopitiliza, Manzi wa Kibera amepakia video kadhaa kwenye instagram yake akiwa na gari jipya kabisa aina ya Prado TX.

Gari hilo jeusi ambapo limebandikwa jina lake katika nambari za usajili anasema ndio kama mpenzi wake mpya na kuonekana akiwa analizunguka akitingika kando kando nalo huku wakiwa na mpenzi wake Chali wa Kibera.

Bado haijajulikana kama ukweli gari ni lake kama ambavyo amedai lakini anaonekana akiwa amelipamba kabisa kwa jina lake sehemu zote mbili za nambari ya usajili.

Haya yanajiri miezi kadhaa baada ya kupakia video akiwa katika nyumba ya matope ambapo alikuwa analia kwamba watu wamemtumika katika umaarufu lakini maisha yake bado hayajapata unafuu.

Madai ambayo mkuza maudhui Eve Mungai aliyakanusha na kutishia kumwaga ukweli wa mambo paruwanja endapo mwanamitindo huyo wa Kibera angeendelea kudanganya watu kwamba anaishi hali ya umaskini.

Suala hilo lilisababisha mkwaruzano mkali mitandaoni baina ya hao wawili huku Manzi wa Kibera akimtaka Mungai kuzifuta video zake kwenye chaneli yake ya YouTube ambazo aliwahi mfanyia mahojiano.