'Asiwahi ita jina langu tena,'Hatimaye Eric Omondi amjibu Notiflow

Muhtasari
  • Aliwataka wasanii kuishi kulingana na uwezo wao wala sio kufanya vitu ili kuufurahisha umma na kuwapiga vita wasanii wenzao
Image: INSTAGRAM// ERIC OMONDI

Baada ya Notiflow kumshambulia na kumsuta mcheeshaji maarufu nchini Eric Omondi baada ya kumnunulia mpenziwe gari, Eric amejitokea wazi wazi na kumjibu.

Notiflow kupitia ujumbe aliochapisha katika insta story yake, alisema kwamba mastaa wengi wanaiga kitendo chake cha kumzawidi mpenziwe gari ili kuwafurahisha mashabiki ila yote ni uongo.

Aliwataka wasanii kuishi kulingana na uwezo wao wala sio kufanya vitu ili kuufurahisha umma na kuwapiga vita wasanii wenzao ambao wanafanya mambo makubwa.

"Yangu ni mnunulie msichana wangu ggari, kila mtu amekuwa aiaribu kuthibitisha jambo, ati Eric amemnunulia mpenzi wake gari mara kitanda cha mtoto wangi kinagharimu elfu 300,"Notiflow Aliandika.

Kwa upande wake Erick Omondi alimtaka Notiflow kukoma kumtaja kwa kuwa hawapo kwenye viwango sawa.

"Ambieni huyo chokora asiwai ita jina yangu tena," Omondi aliandika.

Notiflow alipakia logbook ya gari alilolinunua katika mtandao wa Instagram, kuonyesha uhalisia wa kitendo chake.