"Amempata!" Ndugu ya Diamond Platnumz afunguka kuhusu mipango ya ndoa yake

Muhtasari

•Momo alidokeza kwamba mke mtarajiwa wa Diamond ni mtu mashuhuri na kueleza kuwa moyo wake tayari umeridhika na malkia huyo wake mpya.

Diamond na msanii wake Zuchu ambaye anadaiwa kuwa kwenye mahusiano naye
Diamond na msanii wake Zuchu ambaye anadaiwa kuwa kwenye mahusiano naye
Image: KWA HISANI

Ndugu mkubwa wa Diamond Platnumz, Ricardo Momo alishiriki mazungumzo ya simu na mtangazaji Juma Lokole siku ya Jumanne.

Momo ambaye pia ni meneja katika lebo ya WCB alifunguka machache kuhusu harusi inayozungumziwa sana kwa sasa ya Diamond na malkia asiyetambulishwa.

Ndugu huyo wa Diamond alifichua kwamba msanii huyo alipokea msala wa Ramadhan kutoka kwa mpenzi wake.

Momo pia alifichua kwamba tayari Diamond amempata mpenzi wa moyo wake ambaye anakusudia kushiriki maisha yote naye.

"Tuko kwenye mipango ya ndoa. Baadae kila mtu atajua ni lini, saa ngapi na muda gani hili jambo litakuwa midomoni mwa watu. Amempata, tuko kwenye mchakato wa kukamilisha jambo hilo," Momo alisema.

Momo alidokeza kwamba mke mtarajiwa wa Diamond ni mtu mashuhuri na kueleza kuwa moyo wake tayari umeridhika na malkia huyo wake mpya.