'Mwambieni awache kinipa block,'Harmonize asema baada ya kununulia Kajala mkufu wa milioni 5

Muhtasari
  • Harmonize alinunua cheni hiyo kwa Tsh 5Milioni, na akasema ni ya aliyekuwa mpenzi wake Kajala na ana uhakika Kajala atamrudia
Harmonize na Frida Kajala
Harmonize na Frida Kajala
Image: HISANI

Hakika Harmonize yuko kwenye mapenzi na anajaribu kufanya kila linalowezekana ili Kajala amrudie tena.

Baada ya kuomba mitandaoni na hata kuweka bango kwenye moja ya barabara za Tanzania, na bado hajapata majibu kutoka kwa ex wake Kajala, Harmonize ameamua kutumia pesa nyingi zaidi.

Leo tarehe 6 Aprili 2022, Harmonize alienda kwenye duka la vito na akatambua cheni ya dhahabu ambayo Kajala alikuwa akiipenda sana.

Harmonize alinunua cheni hiyo kwa Tsh 5Milioni, na akasema ni ya aliyekuwa mpenzi wake Kajala na ana uhakika Kajala atamrudia.

Harmonize anatumai kuwa Kajala atarejea kama inavyofahamika Harmonize amekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi tofauti baada ya kuachana na Kajala lakini mambo hayakumwendea vyema.

Anadhani kuwa Kajala ndiye suluhisho pekee.

Pia msanii huyo aliwasihi wanamitandao kushauri Kajala awache kumpa block kwenye mitandao ya kijamii.