"Wewe ni wangu wa kwanza na wa mwisho" Diamond amsherehekea mpenziwe baada yake kumzawadia

Muhtasari

•Diamond alipakia kanda za video zilizoonyesha vitu vya sala na zawadi zinginezo kochokocho ambazo alidokeza kanunuliwa na mpenzi wake ambaye hajatambulishwa.

•Baba huyo wa watoto wanne wanaojulikana aliendelea kuhakikishia kipenzi chake kwamba anampenda sana.

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Image: INSTAGRAM

Huku mwezi mtukufu wa Ramadhan tayari ukiwa umeng'oa nanga kirasmi, staa wa Bongo Diamond Platnumz amepokea zawadi maalum kwa msimu huu kutoka kwa mchumba.

Mwanamuziki huyo anayeshabikiwa sana kote duniani alipakia kanda za video zilizoonyesha vitu vya sala na zawadi zinginezo kochokocho ambazo alidokeza kanunuliwa na mpenzi wake ambaye hajatambulishwa.

"Aleykum my habiby, msala huu mzuri nimekupa leo ikuwe ishara na ukumbuhi kwamba Sulah si kwa ajili ya Allah, Salah ni kwa ajili yako yetu sababu sisi tunamhitaji yeye kukiko anavyotuhitaji sisi. Duniani mithili yako hakuna na peponi. Tukakutanishwe  tena. Nakupenda Rouny," Jumbe ambazo ziliambatanishwa na zawadi hizo ulisoma.

Diamond alizamia kwenye ukurasa wake wa Instagram kumsifia mchumba wake kwa makubwa aliyomfanyia. Alionekana kuridhishwa sana moyoni na mpenzi huyo wake wa sasa.

"Kumpata anayekupenda ni jambo moja, ila kumpata atakayekuelewa na kukupa unachotaka ni jambo lingine kabisa," Diamond alisema.

Baba huyo wa watoto wanne wanaojulikana aliendelea kuhakikishia kipenzi chake kwamba anampenda sana.

"Simba anakupenda sana.. Wewe ni wangu wa kwanza na wa mwisho," Alisema.

Haya yanajiri huku uvumi wa harusi ya mwanamuziki huyo  na mchumba huyo wake ukiwa unaendelea kusambaa kote mitandaoni.

Mamake Diamond ameendelea kumshinikiza afunge pingu za maisha na mpenzi  huyo wake baada ya mwezi wa Ramadhan. Mama Dangote ameonekana kuridhishwa na mkaza mwana huyo wake mpya.