Govi wa Machachari akiri kuchumbiana na wanawake wazee kumliko

Muhtasari

•Govi alifichua kwamba miaka yote ya maisha yake amekuwa akichumbiana na wanawake waliompiku umri.

•Mwigizaji huyo pia alikiri kuwahi kuwa kwenye mahusiano kadhaa ambayo yalikosa kufua dafu.

Image: INSTAGRAM// MALIK LEMMY

Mwigizaji Malik Lemmy almaarufu kama Govi kutokana na kipindi 'Machachari' ambacho aliigiza amefunguka mengi kuhusu mahusiano yake.

Govi aliwashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu (Q&A) kwenye mtandao wa Instagram ambap[o alizungumzia masuala mbalimbali kuhusu maisha yake.

Mwigizaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alifichua kwamba miaka yote ya maisha yake amekuwa akichumbiana na wanawake waliompiku umri.

"Mi bora nimekutambua manze na umenitambua. Kwanza maishani mwangu nimekuwa nikuchumbiana na wanawake walionizidi umri," Govi alimjibu shabiki aliyehoji kama anaweza kujitosa kwenye mahusiano na mwanamke mzee kumliko.

Mwigizaji huyo pia alikiri kuwahi kuwa kwenye mahusiano kadhaa ambayo yalikosa kufua dafu.

"Nimekuwa kwenye mahusiano. Nimetoka kwa mengine na pia nimeachwa. La muhimu ni kuwa bado nipo hai," Alisema.

Govi hata hivyo alifichua kwa sasa hayupo kwenye mahusiano yoyote. Hata hivyo alidokeza kwamba kuna mwanadada ambaye amekuwa akiandama.

"Mwanamke ambaye naona kwenye ndoto zangu.. yeye ni asilimia 20 kwa 10. Yeye hutabasamu vizuri na alafu anajua kuvaa," Alimjibu shabiki aliyeuliza kuhusu mwanamke wa ndoto zake.

Muigizaji huyo alisema anaamini katika kutafuta pesa kwanza kabla ya kujitosa kwenye maisha ya mahusiano.