"Nakupenda Rouny" Diamond aandikiwa ujumbe mtamu wa kimapenzi na mchumba wake

Muhtasari

•Zawadi  hizo ziliambatanishwa na ujumbe maalum huku malkia huyo akimhakikishia Diamond kwamba anampenda sana.

•Mama Dangote ameendelea kumshinikiza mwanawe Diamond afunge pingu za maisha na kipenzi hicho chake mwishoni mwa Ramadhan.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Mapema wiki hii mwanamuziki Diamond Platnumz alipakia video na picha za zawadi ambazo alipokea kutoka kwa mpenzi wake ambaye bado hajatambulishwa.

Malkia huyo alimzawadi Diamond kwa msala miongoni mwa zawadi zingine kochokocho kutoka huku mwezi mtukufu wa Ramadhan uking'oa nanga.

Zawadi  hizo ziliambatanishwa na ujumbe maalum huku malkia huyo akimhakikishia Diamond kwamba anampenda sana.

Soma hapa ujumbe wa mpenzi wa Diamond kwake:-

"Aleykum my habiby, msala huu mzuri nimekupa leo ikuwe ishara na ukumbuhi kwamba Sulah si kwa ajili ya Allah, Salah ni kwa ajili yako yetu sababu sisi tunamhitaji yeye kukiko anavyotuhitaji sisi. Duniani mithili yako hakuna na peponi. Tukakutanishwe  tena. Nakupenda Rouny," Ujumbe huo ulisoma.

Mama Dangote ameendelea kumshinikiza mwanawe Diamond afunge pingu za maisha na kipenzi hicho chake mwishoni mwa Ramadhan.

Hivi majuzi Mama Dangote alisema ombi lake kubwa kwa mwanawe kabla hajaaga dunia ni kucheza katika harusi yake.

"Mwanangu Naseeb Diamond Platnumz🦁. Nadhani unajua kilio changu cha kila siku kwako, Natamani nicheze harusi yako kabla sijakata kauli. Ushampata mwenza ndio umuoe Ramadhan ikiisha nawe uwe ndani ya ndoa Mwanangu," Mama Dangote alimwambia mwanawe kupitia mtandao wa Instagram.