Utapenda! Sifa za mwanamke anayeolewa na Diamond

Muhtasari

• Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na tetesi zenye ishara tosha kwamba mara hii msanii Diamond Platnumz yupo tayari kufunga ndoa.

• Japo hadi sasa bado hajaweka wazi jina lake wala anakotokea.

Habari za msanii Diamond Platnumz kufunga ndoa zimekuwa zikitawala anga za taifa la Tanzania na Afrika Mashariki, huku fumbo la kichuna huyo aliyebahatika likisalia kuwa fuumbo.

Wandani wa Simba wameonekana kufahamu mwanamke huyo ila wakadinda kutaja jina lake moja kwa moja.

Sasa Juma Lokole ambaye ni mtangazaji ndani ya Wasafi fm ametoa sifa za mwanamke huyo anayetarajiwa kuolewa na Diamond:

• Mke mtarajiwa wa Simba ni mpishi mzuri

• Ana miguu kama ya Elizabeth Michael

• Ni mnyenyekevu na sio msemaji sana

• Hapendi ugomvi na watu asiowajua

• Ameahidi kuwaheshimu waliokuwa wake wa Diamond Platnumz

• Ni msomi ambaye ana kiasi kizuri cha mali

Ifahamike kwamba hatua hii ya Diamond kutaka kufunga ndoa inajiri wakati ambapo wengi wa mashabiki na washikadau wanakisia kwamba huenda Zuchu akawa ndiye mke rasmi wa Simba.

Mamake Diamond pia ameonekana kufurahikia kitendo hicho huku akimtakia kila la heri na kumsihi asipoteze muda.

Tayari Simba ameshakuwa ndani ya mahusiano zaidi ya matatu ambayo yalisambaratika kwa sababu mbalimbali.

Kwa sasa mashabiki wanasubiria kumuona rasmi mke huyo ambaye amesifiwa si haba.