"Ni mtukutu" Zari Hassan amzungumzia mtoto wake na Diamond Platnumz, Prince Nillan

Muhtasari

•Nillan alikuwa amevalia mkufu wenye maandishi 'WCB' ambayo yanasimamia lebo ya babake, Wasafi Classic Baby.

•Licha ya kutengana kwao, Diamond na Zari bado ni marafiki wakubwa na wanaendelea kushirikiana vizuri katika malezi ya watoto wao.

Image: INSTAGRAM// PRINCE NILLAN

Mwanasoshalaiti Zari Hassan kutoka Uganda ni miongoni mwa wapenzi wa zamani wa staa wa Bongo Diamond Platnumz.

Zari na Diamond walichumbiana kati ya 2014 na 2018 ambapo mahusiano yao yaligonga ukuta na kila mmoja wao akaenda njia tofauti.

Katika kipindi cha mahusiano nayo, wasanii hao walibarikiwa na watoto wawili pamoja, binti mmoja na mvulana mmoja.

Tiffah Dangote alizaliwa mwaka wa 2015 huku mtoto wao wa pili Prince Nillan akizaliwa mwaka mmoja baada ya binti yao.

Licha ya kutengana kwao, Diamond na Zari bado ni marafiki wakubwa na wanaendelea kushirikiana vizuri katika malezi ya watoto wao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari alionyesha jinsi mtoto wake wa pili na Diamond, Prince Nillan amekuwa mkubwa.

Mama huyo wa watoto watano alipakia picha kadhaa za Nillan huku ambaye alionekana mtanashati na mchangamfu . Nillan alikuwa amevalia mkufu wenye maandishi 'WCB' ambayo yanasimamia lebo ya babake, Wasafi Classic Baby.

"Kwa nini anaonekana mzuri lakini mtukutu," Zari aliandika chini ya picha hizo za Nillan.

Mara kwa mara Diamond hufunga safari ya kuelekea Afrika kusini kuwaona watoto wake na Zari. Diamond ameonekeana kuwapendelea zaidi watoto hao wake na mwanasoshalaiti huyo wa Ugnanda.