Baadhi ya watu maarufu ambao wamebarikiwa na watoto mwaka huu

Muhtasari

•Robo ya kwanza ya mwaka imekuwa ya baraka kwa baadhi ya wasanii wa Kenya ilhali wengine wamekumbwa na masaibu mbalimbali.

•Mwanamuziki Everlyn Wanjiru alitangaza habari njema kuhusu ujauzito wake wa kwanza baada ya kusubiri kwa takriban miaka kumi

Karen Nyamu, Kabi Wajesus, Nadia Mukami
Karen Nyamu, Kabi Wajesus, Nadia Mukami
Image: HISANI

Miezi mitatu na nusu tayari imepita tangu tulipouzindua mwaka huu wa 2022.

Robo ya kwanza ya mwaka imekuwa ya baraka kwa baadhi ya wasanii wa Kenya ilhali wengine wamekumbwa na masaibu mbalimbali.

Tumeshuhudia baadhi ya wasanii mashuhuri  wakibarikiwa na watoto huku wengine wakitangaza ujauzito.

1. Nadia Mukami na Arrow Bwoy

Wanandoa maarufu Nadia na Arrow Bwoy walibarikiwa na mtoto wa kiume mnamo Machi 24, 2022. 

Wawili hao walimpatia mtoto wao wa kwanza jina Haseeb Kai.

2. Kabi na Milly Wajesus

Wanavlogu Milly na Kabi wa The Wajesus Family walitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili mnamo Aprili 8, 2022.  

Kabi na Milly walifichua kwamba binti yao alizaliwa siku chache kabla yao kutangaza hadharani. Hata hivyo bado hawajakubaliana kuhusu jina la kumpatia mtoto wao.

3. Karen Nyamu 

Mwanasiasa na wakili mashuhuri Karen Nyamu alibarikiwa na mtoto wake wa tatu mnamo Februari 26, 2022.

Nyamu alijifungua mtoto wa kike ambaye alipatia jina Njeri.

Inaaminika kuwa staa wa Mugithi, Samidoh ndiye baba ya mtoto huyo wa Nyamu. Wawili hao wana mtoto mwingine wa kiume pamoja.

Siku ya Jumanne, mwanamuziki Everlyn Wanjiru alitangaza habari njema kuhusu ujauzito wake wa kwanza baada ya kusubiri kwa takriban miaka kumi. Kumekuwa na ripoti zilizotokea kuwa huenda mke huyo wa Agundabweni Akweyu tayari amejifungua.

Mwanamuziki Juliani na mke wake Lilian Ng'ang'a wanaripotiwa kutarajia mtoto wao wa kwanza pamoja baadae mwaka huu. Ingawa wawili hao bado hawajajitokeza kutangaza, mapema mwaka huu Bi Lilian alionekana akiwa amebeba ujauzito.

Wasanii wengine ambao wanatarajia mtoto ni pamoja na mwigizaji Jackie Matubia na mpenzi wa mwigizaji Tyler Mbaya almaarufu Baha.