[Video] Wakazi wa Homabay walalamikia ukosefu wa 'password', katika mtambo wa kura za mchujo

Muhtasari

• Wakazi wa kaunti ya Homabay wamelalamikia ukosefu wa password katika mtambo wa kupiga kura za mchujo.

• Walisema kwamba kulikuwa na njama ya kuhitilafiana na shughuli hiyo.

Shuguli ya kura za mchujo ikiendelea
Shuguli ya kura za mchujo ikiendelea
Image: Onyango Ochieng

Wakazi katika kaunti ya Homabay wameonyesha kughadhabishwa kwao baada ya nywila [password] ya mashine walizopaswa kutumia katika kupiga kura za mchujo za chama cha ODM  kukosekana.

Kulingana nao, walipewa taarifa kwamba password hiyo ingesafirishwa kwa gari hadi katika maeneo ya kupigia kura hizo za mchujo.

Walisema kwamba kulikuwa na uongo mwingi na njama za kuhitilafiana na mchakato huo.

"Kama hii shughuli ni ya kidijitali, mbona watume password kwa gari?" Mmoja wa wakazi aliuliza.