Rayvanny na Fahyvanny washerehekea siku ya kuzaliwa ya mwanao kwa njia ya kipekee

Muhtasari
  • Rayvanny na Fahyvanny washerehekea siku ya kuzaliwa ya mwanao kwa njia ya kipekee

Kama wengi wanavyojua na kufahamu ni kuwa staa wa bongo Rayvanny na baby mama wake walitengana kwa sababu moja ua nyingine.

Baada ya kutengana kwao Rayvanny aliendelea na maisha yake huku akianzisha uhusiano wa kimapenzi na Paula Kajala.

Uhusiano wa waili hao ulikejeliwa na wengi, huku lawama ikimwendea Paula kwani wengi walidai kwamba alivunja familia ya wenyewe.

Leo ni siku ambayo mtoto wao anatimiza mwaka mmoja zaidi. Ambayo ameingia kwenye mtandao wake wa kijamii na kumwandikia ujumbe maalum, akimtakia kila la heri maishani.

Ujumbe huo ulisomeka;

"Young tiger, love you so much son, Happy birthday my G."

Rayvanny aliachana na baby mama yake kitambo lakini tetesi zilienea kuwa wamerudiana. Ingawa alikuwa akimchumbia  Paula Kajala

Kutengana kwao hakujawazuia wawili hao kumsherehekea mtoto wao huku Fahyvanny akimwandikia ujumbe  mtoto wake na kumwambia kwamba anampenda sana.

"Heri ya kuzaliwa mtoto wangu, nakupenda sana," Aliandika Fahyvanny.