Nilimcheza Stivo Simple Boy na wababa na sijuti- Aliyekuwa mpenzi wake Stivo afichua

Muhtasari
  • Baada ya kutangaza kuachana kwao, Pritty anasema wanaume wazee zaidi wanamtumia jumbe kwenye mitandao ya kijamii
Pritty Vishy, Stivo Simple Boy
Pritty Vishy, Stivo Simple Boy
Image: INSTAGRAM

Mpenzi wa zamani wa Stivo Simpleboy Pritty Vishy amefunguka kuhusu kumcheza mwimbaji huyo bila yeye kujua.

Akiwa kwenye mahojiano na Mpasho Pritty alisema kuwa aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wazee, na Stivo hakuwahi kufahamu hilo.

Pritty, ambaye alianza kuchumbiana na Stivo mnamo 2019 aliongeza kuwa alikuwa na 'Wababa' 3 na wangemdekeza zaidi ya mwimbaji huyo angeweza.

“Mimi nilishawahi kumcheza, lakini na Mubaba (mzee) Wababa 3. Wababa walikuwa wakinidekeza, Stivo hakujua. Sijisikii hatia, hakuna nafasi ya kujuta. " alisema

Baada ya kutangaza kuachana kwao, Pritty anasema wanaume wazee zaidi wanamtumia jumbe kwenye mitandao ya kijamii.

"Kuna Wababa kwenye DM yangu, wengine ni wazee sana. Lakini nilirekebisha, siwezi kurudi nyuma. DM yangu imejaa sani

Aliheshimu uhusiano lakini ilifikia hatua akawa mnene. Stevo ni mtu ambaye unaweza kumuelewa tu baada ya kukaa naye kwa muda."

Kuhusu iwapo anaweza kumsamehe Stivo, Pritty anasema;

"Nataka ajue thamani yangu. Akae chini na kufikiria kama ni mimi au mtu mwingine. Nataka itoke moyoni mwako."

Hata hivyo, alibadilisha marafiki zake punde tu baada ya kupata umaarufu kwa sababu walianza kuwa na matarajio makubwa kutoka kwake.