Burning Spear adokeza kufanya tamasha la Reggae Kenya

Muhtasari

• Mwanamuziki mkongwe kutoka Jamaica Burning Spear amedokeza kufanya tamasha la muziki nchini kenya hivi karibuni.

Msanii mkongwe wa mitindo aian ya Reggae, Winston Rodney almaarufu Burning Spear amedhibitisha kwamba hivi karibuni ataisimamisha nchi ya Kenya kwa kufanya tamasha kubwa ambalo halijawahi kushuhudiwa kutoka kwa wasanii wa Reggae tokea Jamaica.

Burning Spear alidhibitisha hili kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo aliwauliza Wakenya kama wako tayari kwa ujio wake wa kishindo.

Msanii huyo mkongwe ambaye ni miongoni mwa waanzilishi wa Reggae na ambo wako hai aliendeleza msururu wa mataifa ambayo angependa kufanya ziara yake ya kimuziki, akiletwa na waandalizi wa matamasha kama vile Reggae Lake festival, Jamrock Reggae Cruise na Rototom Sunsplash.

Kulingana na mpangilio alioudokeza kwenye facebook yake na ambao haijabainika wazi kama ndio utakuwa mpangilio rasmi, Burning Spear alidokeza kuanza na Kenya, Ethiopia, Afrika Kusini, Ghana na Uingereza.

“Salamu Kenya, ndio salamu Ethiopia na South Africa, mko tayari? Salamu Ghana na bara zima la Afrika, baraka mfululizo. Salamu London, Birmingham mko tayari kweli, zungumza na mimi tafadhali, niko tayari,” aliandika Burning Spear.