India: Wawindaji haramu wanaswa wakimbaka kenge (Monitor Lizard)

Muhtasari

• Wawindaji haramu wanne nchini India walifanya kufuru ya karne baada ya kuonekana kwenye video wakimbaka kenge aina ya Bnegal Monitor Lizard.

Pingu
Image: Radio Jambo

Duniani kuna mambo ya kustaajabisha katika kila sekunde iendayo kwa Mungu. Na mengi ya matukio haya husababishwa na watu.

Taarifa zilizosambaa kutoka nchini India wikendi iliyopita ziliwaacha wengi katika mshangao mkubwa baada ya madai kwamba wanaume wanne wawindaji walifanya kitendo cha aibu cha kumbaka mnyama aina ya kenge.

Mamlaka ya uhifadhi wa wanyamapori katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu ilidaiwa kuwazuilia wawindaji hao ambao walitiwa hatiani baada ya uchunguzi wa kina katika simu ya mmoja wao kuonesha kwamba alikuwa amechukua video ya wenzake wakitendo kitendo hicho cha aibu kwa mnyama huyo asiye na hatia.

Mamlaka zimesema ziliingiwa na shaka na kwa bahati ziliweza kuwafuatilia kupitia kamera maalum(cctv) zilizopo hifadhini humo.

Watuhumiwa hao wanne waliotambulika kwa majina yao Sandeep Tukram, Pawar Mangesh, Janardhan Kamtekar na Akshay Sunil walitiwa nguvuni na kuzuiliwac ambapo uchunguzi sasa unaendelea ili kubaini kama ni wote walifanya kitendo hicho kinachoonekana kwenye kamera.

Iwapo watapatikana na hatia, watahukumiwa kifungo kisichozidi miaka saba jela.

 

Kenge aliebakwa kwa zamu ni aina ya kenge wakubwa wanaojulikana kama bengal monitor lizards ambao ni moja ya viumbe vinavyolindwa sababu ya kuwa hatarini kutoweka katika uso wa dunia.