Kijana afumaniwa kwa kina binti, avunjwa miguu na mikono

Muhtasari

• Kijana mmoja nchini Tanzania anaendelea kuuguza majeraha baada ya kufumaniwa kwa kina binti akitaka kushiriki ngono.

Crime Scene

Tamaa ya kijana mmoja ya kutakqa kuchovya asali ya mzinga katika boma la mwenyewe ilimsababishia kilema baada ya kufumaniwa na kukabidhiwa kipigo kikali mithili ya walokole wanavyomshambulia shetani wakati wa maombi.

Kijana huyo mdogo aliyetambulika kwa jina Benard Mkolwe kutokea mkoa wa Njombe nchini Tanzania alikipata baada ya kufumaniwa na msichana wa shule kwa jina Sara ambaye alikuwa amemchumbia kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuamua kutia miadi ya mapenzi ntumbani kwao msichana.

Baada ya mipango yao kutibuliwa, kijana alipigwa kitutu hata baada ya kukiri kwamba ndio mara ya kwanza alikuwa anajaribu kufanikisha azma ya kukata kiu chake cha mapenzi lakini kujitetea kwake kukawa kunaangukia kwenye maskio ya kiziwi.

“Wakati wananipiga wakaniambia kwanini unatembea na binti yetu nikawaomba samahani nimekosa lakini hawakutaka kunielewa” alisema Benard Mkolwe

Kulingana na taarifa iliyochapishwa na kituo kimoja cha habari nchini humo, kijana huyo alisema kwamba baba zake wadogo na msichana huyo ndio walimshambulia vikali kwa kutembea na msichana wao hata baada ya kusema hajawahi toka na yeye kimapenzi na hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza na ambayo haikufanikiwa.

“Waliofanya tukio ni baba zake wadogo wa yule binti yule binti ni kama wiki mbili tuko kwenye mahusiano lakini sijawahi kufanya kitu chochote kile tulikuwa ni marafiki wa kuchati na ile siku alivoniita nahisi ndio ilikuwa siku ya kuelekea kwenye tendo lakini sikufanya kitu chochote” aliongeza Mkolwe.

Kwa sasa kijana huyo aliyevunjwa vunjwa vibaya mno anaendelea kupata matibabu katika hospitali moja nchini humo.

Ni kitendo ambacho kinasemekana kupingwa vikali na mkuu wa wilayani himo ambey alisema vijana hao kama si kuelewana basi huyo kijana asingekuja mpaka kwao kina binti.

“Labda kuna visa vya awali,huu ni ukatili wa kijinsia unaotokana na binti kusuka mpango kumuonea huyu kijana,yeye amekubali kuchati halafu wanakuja kumpiga na kama alikuwa hana uhitaji wa kukutana na huyu kijana angemkatalia toka mwanzo” alisema mkuu wa wilaya.