Mchuuzi aliyemwagiwa chakula na 'kanjo' akutana na mkuu wa mkoa na kusherehekea pasaka pamoja

Muhtasari

• Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alimualika nyumbani kwake jamaa ambaye kanjo walimwaga chakula chake cha kuchuuza

• Kanjo wa mji wa Mwanza walimwaga ndizi za mchuuzi huyo juzi, kitendo ambacho kilizua hasira kali miongoni mwa watu.

Image: MARGARET WANJIRU

Tumaini Saimon Mkono ambaye ni mfanyibiashara wa bidhaa ndogo ndogo kutokea jiji la Mwanza nchini Tanzania ni mtu mwenye furaha zaidi ambaye anawexza kutumia kurasa zaidi ya alfu kuelezea maana halisi ya methali ‘baada ya dhiki ni faraja’

Mfanyibiashara huyo ambaye kwa jina lingine wafanyibiashara wa namna hiyo wanaitwa machinga wa kuchuuza bidhaa aligonga vichwa vya habari siku chache nyuma baada ya ‘kanjo’ wa jiji la Mwanza kuchukua na kumwaga ndizi zake alizokuwa akichuuza kwa ajili ya kujitafutia riziki.

Inaarifiwa kitendo hicho kiliwaghadhabisha watu wengi baada ya kuonekana mitandaoni na ambapo kilifikia mpaka uongozi wa mkoa wa Mwanza ulioamrisha wote waliohusika kuhujumu riziki ya kijana huyo kuchukuliwa hatua.

Siku ya pasaka, mkuu wa mkoa huo wa Mwanza alimtafuta jamaa huyo mchuuzi wan dizi na kumualika nyumbani kwake ambapo walisherehekea pasaka pamoja kwa chakula.

 

Hatua wa RC huyo wa mkoa kuhakikisha kwamba wote waliohujumu biashara ya bwana Mkono walichukuliwa hatua na pia kumtafuta kwa ajili ya kusherehekea pampja ilisherehekewa sana ambapo wengi walimpongeza kwa kusema kwamba kweli huo ndio utumishi kwa wote.

"Nampongeza Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi kwa kuchukua hatua ndani ya saa 24 niliyomuagiza. Kitendo hicho cha kikatili na cha kukosa utu kilinikwaza sana ningekuwa Mwanza mtu angekula hedi. Wakuu wa mikoa endeleeni na zoezi la kutenga maeneo rafiki kwa biashara ya Machinga, kuyawekea miundombinu rafiki, kuwapanga kwenye maeneo kwa utaratibu unaoheshimu utu, kuwapa elimu ya biashara na kuwaunganisha na bima na taasisi za fedha, na kuepuka kuendesha opereshi zinazoepuka uharibifu wa mali," wanahabari walimnukuu Mheshimiwa Bashungwa akifoka.