"Mapenzi hi uongo!" mwanamke agundua mchumba wake kwa miaka 2 yuko kwenye ndoa ya miaka 6

Muhtasari

• Mwanamke huyo alijuta kwa kuchumbiana miaka miwili na mwanaume aliyekuwa kwenye ndoa ya miaka 6 na watoto wawili juu.

Mhasiriwa wa dhuluma za kijinsia
Image: THE STAR

Mwanamke mmoja kwenye mtandao wa Twitter ameachia ujumbe wenye ukakasi mkubwa baada ya kudai kwamba mchumba wake wa kiume ambaye wamekuwa katika mahusiano ya uchumba kwa miaka miwili alikuwa ameoa kwa miaka 6 sasa pasi na mwanamke huyu kujua.

Alielezea kwamba amekuja kugundua kwa kuchelewa kwamba mpenzi wake huyo wa miaka miwili bado yupo kwenye ndoa ya miaka sita ambapo ana watoto wawili tayari na mke wake halali wa ndoa.

Mwanamke huyo kwa jina Mama Bear aliandika kwa masikitiko makubwa jinsi amekuwa akimuombea mwanaume huyo usiku na mchana ili kufanikiwa maishani na baadae kufunga ndoa naye kumbe jamaa huku amekuwa akichepuka tu na nyumbani ana ndoa ya miaka 6 na watoto wawili juu.

“Nimekuja kugundua tu kwamba mchumba wangu wa miaka miwili ako katika ndoa ya miaka sita na watoto wawili. Siwezi hurumia machozi yangu machozi yangu. Kwa usiku zote nimekuwa nikimuombea na kumpa moyo wangu wote, ni sawa tu, pengine simtumikii Mungu aliye hai,” binti huyo aliandika kwa maskitiko.

Mwanamama huyo aliyeonekana kuvunjika moyo vipande vipande aliendeleza kunung’unika kwamba mwanaume huyo asiye na aibu mpaka alivuka safu za juu zaidi ambapo alikuwa mpaka anazungumza na dada zake pamoja na mama yake na kuwaahidi ndoa naye.

“Unazungumza na mamangu pamoja na dada zangu ukiwaahidi ndoa na mimi, ninazungumza na familia yako, aje? Mpaka ninakusaidia kurembesha nyumba yako… sehemu ya nafsi yangu bado inahisi hii ni ndoto,” aliandika kwa majonzi makubwa Mama Bear.

Kama ilivyotarajiwa, watu wengi waliofuatilia thread hiyo walitoa maoni yao mbali mbali baadhi wakimhurumia huku wengine wakimtupia maneno makali kwa kujipa sana bila kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mwanaume huyo.

Ila yeye alisisitiza kwamba katu hamlaumu mwanaume yule kwa kitendo chake hicho bali anajilaumu mwenyewe kwa kutomjua vizuri.

“Nyinyi wote hamnielewi. Mimi simlaumu mwanaume yule, ningemjua tu vizuri. Hata mama yangu alimkubali mno pamoja na tabia zake njema kumbe mapenzi hayapo tena, sidhani kama mapenzi yapo duniani, ni uongo mtupu,” aliandika mwanamama huyo.