Mwanaume Muislamu atoroka ndoa, amlaumu mkewe kwa manyanyaso ya kimwili, kihisia

Muhtasari

• Merbaan Talib alieleza kwamab maji yalipozidi unga katika ndoa yake, aligura na kutokana na kunyanyaswa na mkewe.

• Alimlaumu mkewe kwa kumnyanyasa kifikira, kihisia, kwa maneno na kimwili pia.

Mwanaume aliyevunjika moyo wa mapenzi
Mwanaume aliyevunjika moyo wa mapenzi
Image: THE STAR, MOSES SAGWE

Mwanaume mmoja kwa jina la Merbaan Talib kwenye mtandao wa Twitter ameamua kufunguka na kueleza wazi kiini cha kuitoroka ndoa yake, kinyume na mafunzo ya dini yake ya Kiislamu.

Talib alielezea kwamba aliamua kuiasi ndoa yake ya muda mrefu kutokana na mateso dhidi yake kuzidi kutoka kwa mke wake ambaye kulingana na mwanaume huyu alikuwa anamnyanyasa kihisia, kimwili na pia kupitia maneno.

“Kama mwanaume Muislamu, pengine nitakuwa mmoja kati ya wale wachache ambao huzungumza, ila nitazungumza tu. Nilimuacha mchumba wangu kwa sababu nilikuwa nanyanyaswa katika kipindi chote cha ndoa yetu. Ninaposema kunyanyaswa namaanisha kwa maneno, kwa hisia na ndio, kimwili. Kamwe siwezi nyamaza kwa wanaume ambao pia hunyanyaswa,” aliandika Talib.

Katika Tweet hiyo ambao imezua gumzo pevu kwa wiki moja sasa, wengi walifurika hapo wakisema kwamba wanaume wengi tu huteseka na kunyanyaswa katika ndoa zao ila wa kuzungumza kwa niaba yao hayupo kwani wakati wote wanaume wanaonekana kutoka upande wa wakosaji, hata kama ni wao wamekosewa.

“Hili ni gumzo pevu na zuri sana ambalo kwa kawaidqa jamii inaliona kama mwiko, dhana ambayo si kweli. Wanaume huteseka pia,” mmoja aliandika.