[Video] Mshirika ampiga makofi mhubiri aliyetaka kumtoa mapepo

Muhtasari

• Kanda ya video imesambaa mitandaoni ikionyesha mwanamke akimpiga mhubiri makofi kwa kujaribu kumtoa mapepo.

• Washirika wengine walisalia katika hali ya wasiwasi wasijue la kufanya.

Kanisa
Kanisa
Image: BIBLE STUDY TOOLS

Mshirika mmoja amempiga makofi mhubiri ambaye alijaribu kumtoa mapepo.Mwanamke huyo alionekana kudinda kufuata maagizo ya mhubiri huyo ambaye alikuwa akijaribu kukemea mapepo.

Baadhi ya wanamitandao walionekana kumkashifu mhubiri huyo wakisema kwamba ni mtumishi wa uongo.

Wengine walisema kwamba anapaswa kutafuta mafuta ya upako kabla ya kuanza kukemea mapepo.

Mwanamke huyo alionekana kudinda kufuata maagizo ya mhubiri huyo ambaye alikuwa akijaribu kukemea mapepo