Diamond - Damu yangu ni moto, nilijua hatungedumu na Zari, nilikuwa 'player'

Muhtasari

• Diamond alifichua kwamba alikuwa anajua mapenzi yake na Zari hayangedumu licha ya kumzalia watoto wawili.

• Alisema kwa kuwa yeye ni msanii anajumuika na wanawake wengi, na kwamba anapenda wanawake sana.

Zari Hassan, Diamond Platnumz
Zari Hassan, Diamond Platnumz
Image: Facebook///DiamondPlatnumz

Hatimaye msanii Diamond Platnumz amekizungumzia chanzo cha mahusiano yake na mwanamama kutokea Uganda Zari Hassan kuvunjika licha ya wawili hao kujaaliwa watoto wawili.

Akielezea kuhusu kile kilichomkuta katika ile filamu ya uhalisia ya Netflix ambayo imshirikisha, Diamond alisema kwamba alihadithia mmoja kati ya watu walioshiriki pale hadithi ya ukweli kuhusu mahusiano yake akitegemea kwamba angemshauri abadilike na kuboresha mahusiano na familia yake kumbe yule msanii alikuwa na njama ya kumzunguka.

Diamond alisema kwamab alielezea ukweli kwamba tangu mwanzo alikuwa anajua kabisa fika kwamba mahusiano yake na Zari hayangeenda popote licha ya kumpenda sana Zari.

Alielezea hilo kwa Rafiki yake huyo waliyeigiza naye na mambo yakamgeukia.

“Nilimwambia udhaifu wangu kwamba bwana tatizo langu mimi ni mtu wa watotoz, bado damu yangu inachemka na huyu mwanamke (Zari) namheshimu sana. Nampenda sana na amenizalia watoto wawili, watoto ambao nawapenda na najua kwa namna moja au nyingine tukiamua kwamba tuwe pamoja kama wapenzi kwenye ndoa, nitakuwa namdisappoint sana,” alieleza bayana Diamond Platnumz.

Alisema hilo ndio tu analinda mipaka yake kwa sababu akimuangusha katika hilo basi huenda watagombana, kuchukiana na hata kushindwa kulea watoto.

Staa huyo wa Bongo Fleva alisema kwamba heshima yake kwa Zari ni kubwa hadi kuna wakati alikuwa akifika na kama kuna mtu Diamond yupo naye kipindi hicho katika mahusiano alikuwa anamweka pembeni na muda wote kuuelekeza kwa Zari kumdekeza kama malkia vile.

Pia Diamond alikubali kwamba yeye alikuwa na hulka ya kuwachezea wanadada na kisha kuwaacha lakini akalainisha mambo kwa kusema kwamba kwa sasa alishabadilika na kuacha tabia hiyo.