"Marehemu aende kuzimu kujumuika na watundu wenzake!" Tangazo la kifo lazua gumzo

Muhtasari

• Tangazo la kifo limezua gumzo baada ya kumzungumzia kwa mabaya marehemu mpendwa wao 

Kumbukumbu ya tangazo la kifo
Kumbukumbu ya tangazo la kifo
Image: Faceboo// Kundi la Hapo Zama za Kale

Wahenga walisema kwamba usimzungumzie kwa mabaya mtu aliyefariki dunia, na ndio chanzo cha ule msemo wa watu wasiopenda kusifiwa kwa kusema kwamba usinisifie mimi sio maiti. Siku zote, maiti sharti asifiwe kwa mazuri aliyoyafanya enzi za uhai wake, hata kama mabaya yake yalikuwa mia, basi zungumzeni lile zuri moja basi!

Lakini kwa familia moja, ni kinaya.

Familia ya mwendazake Elizabeth Mueni Ngotho ilizua mjadala mkali katika mtandao wa Twitter kutokana na tangazo la kifo chake ambalo walilipia kuwekwa kwenye gazeti moja la humu nchini.

Familia hiyo ilionekana kuwa na tofauti kubwa sana na mwendazake ambapo kwa maneno yao walimtaka aende kujuika na watangulizi wake ambao walishirikiana kufanya njama fulani ambayo haikupendeza wakati wa uhai wao.

“Mueni sasa ameungana na wenzake marehemu babake mpendwa na mshirika mwenza katika uhalifu Peter amabye ni ndugu yake na sasa wanaweza endeleza ukora na utundu wao kutoka pale walipoachia,” sehemu ya kumbukumbu hiyo ya kifo ilisoma.

Wengi walishindwa kujua ni nini haswa familia hii ilikuwa inamaanisha kwa kuanika maovu na mabaya na binti huyo katika tangazo la umma.

Baadhi waliibuka na udadisi mkali na kudai kwamba Mueni alikuwa ni binti wa fundi manyumba mhandisi A.A Ngotho aliyeunda mpango wa ujenzi wa jumba la serikali jijini Nairobi, Nyayo House ambapo ilisemekana hayati rais Daniel Arap Moi alimshrutisha kujenga chumba cha mateso cha chini kwa ajili ya kuwahukumia mahasidi wake wa kisiasa enzi wa utawala wake.