Kilio cha Haki: Wakenya wataka haki kwa msagaji aliyebakwa na wanaume 6 kabla ya kuuawa

Muhtasari

• Sheila Lumumba, 25 ni msagaji aliyebakwa na kundi la wanaume 6 na kisha wakamuua.

• Mauaji yake yamezua maandamano mitandaoni huku Wakenya wakitaka haki itendeke

msagaji Sheila Adhiambo Lumumba
msagaji Sheila Adhiambo Lumumba
Image: Twitter

Mitandao ya kijamii nchini Kenya Ijumaa ilifurika maandamano ya watu wakiteta kuhusu kifo cha mwanamke mmoja ambaye ni msagaji aliyebakwa kabla ya kuawa nyumbani kwake.

Taarifa hiyo ilifichuliwa na mwanaharakati wa kupinga dhuluma za kijinsia, Njeri wa Migwi ambaye alisema kwamba mwanamke huyo msagaji kwa jina Sheila Lumumba alipatana na umauti wake wakati kundi la wanaume sita walivizia nyumbani kwake mjini Karatina na kumbaka kwa zamu, kumvunja mguu na kisha kumuua kwa sababu eti yeye ni msagaji.

Taarifa hiyo Migwi aliyoichapisha kwenye mtandao wake wa Facebook ilizua ghadhabu miongoni mwa Wakenya wengi wakilaani kitendo hicho na kutaka uchunguzi wa haraka ufanyike ili Sheila apate haki japo ni marehemu.

“Wote mimi na Sheila tuna miaka 25 na sisi ni wasagaji. Siwezi tulia kwa sababu pia mimi niko takwimu moja mbali na kuwa mhanga wa kitendo hiki. Siwezi tulia kwa sababu najua mauaji ya Sheila yatakwisha bila kuadhibiwa,” mmoja kwa jina Protect Queer Kenyans aliandika kwenye Twitter.

msagaji Sheila Adhiambo Lumumba
msagaji Sheila Adhiambo Lumumba
Image: Twitter
msagaji Sheila Adhiambo Lumumba
msagaji Sheila Adhiambo Lumumba
Image: Twitter
msagaji Sheila Adhiambo Lumumba
msagaji Sheila Adhiambo Lumumba
Image: Twitter