Milly Chebby afichua sababu ya kuacha kazi katika ofisi ya naibu rais

Muhtasari
  • Milly Chebby afichua sababu ya kuacha kazi katika ofisi ya naibu rais
Milly Chebby
Image: Milly Chebby/INSTAGRAM

Milly Chebby ni miongoni mwa wauna maudhui ambao wanafahamika sana nchini na wanamitandao kutokna na bidii ya kazi yake.

Pia  ni miongoni mwa waunda maudhui amao ni wa kupigiwa mfano mwema na wanamitandao.

Katika Mahojiano na SPM Buzz, mtayarishaji wa maudhui Milly Chebby alifichua kwamba aliwahi kuajiriwa na serikali kabla ya kujiuzulu ili kuzingatia kazi yake ya ushawishi.

Amefichua kuwa alifanya kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu na baadaye Ofisi ya Naibu Rais, wote wawili waliwahi kuwa Idara ya Mawasiliano ya Umma.

“Nilikuwa katika idara ya uhusiano wa umma katika Afisi ya Waziri Mkuu na kisha afisi ya naibu rais William Ruto. Hapo ndipo nilipojiuzulu,” alisema.

Milly alieleza kwamba alijiuzulu kwa sababu kazi hiyo ilikuwa ya kuchosha.

"Nilijiuzulu kwa sababu binafsi, napenda changamoto. Kila siku ninapenda kuamka kwa kitu kipya. Sipendi ubinafsi ulio dhahiri na kuweka alama na hakuna ukuaji wowote… Kuna nyakati ningefika ofisini saa 10:00 a.m. kwa sababu sikuwa na motisha,” alisema.

Mtayarishaji wa maudhui anaongeza kuwa hajutii chochote kutokana na malipo yake kuwa kidogo.

Milly ameolewa na mcheshi na mshawishi Terrence Creative.