'Mpira umerudi kwa kipa,'Fahyvanny ajibu madai ya kurudiana na Rayvanny

Muhtasari
  • Wawili hao waliachana mwaka mmoja uliopita, huku msanii huyo aiendelea na masiha ya mapenzi yake na Paula Kajala

Fahyvanny ni mwanasosholaiti wa Tanzania ambaye anafahamika sana mitandaoni, kwani alikuwa mpenzi wake staa wa bongo Rayvanny.

Wawili hao waliachana mwaka mmoja uliopita, huku msanii huyo aiendelea na masiha ya mapenzi yake na Paula Kajala.

Uvumi umekua ukienea mitandaonikwamba wawili hao wamerudiana, hii ni baada ya wawili hao kutumia muda wao mzuri kusherehekea siku ya kuzaliwa na mtoto wao.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Fahyvanny wa instagram amedokeza kwamba wengi wamekuwa wakiuliza kama wamerudiana au amepata mwanamume mwingine.

Huku akijibu madai hayo Fahyvanny amesema kwama mpira umerudi kwa kipa, ila hajaweka wazi kama wamerudiana.

"Jamani maswali yamekua ni mengi kama nimerudiana na mzazi mwenzangu au nina mpya 🙈 Mpira umerudi kwa keper 🤣🤣🤣 huu mchezo hauitaji hasira 😎," Aliandika Fahyvanny.

Je wawili hao wameridiana, bada ya Rayvanny kuachana na Paula Kajala?