Manzi wa Kibera akiri alitumia dawa kuongeza makalio yake

Muhtasari

•Kipusa huyo aliyekuja kutambulika zaidi mwaka jana amefichua kuwa alitumia dawa kuongeza saizi ya makalio yake.

•Dawa alizokuwa anatumia zilifanya upande mmoja wa makalio yake kuwa mkubwa zaidi kuliko ule mwingine.

Image: INSTAGRAM// MANZI WA KIBERA

Mwanasoshalaiti maarufukutoka mtaa wa Kibera, Manzi wa Kibera amekiri kuwa makalio yake sio ya asili kabisa.

Kipusa huyo aliyekuja kutambulika zaidi mwaka jana amefichua kuwa alitumia dawa kuongeza saizi ya makalio yake.

"Matako yangu sio kutoka kwa Mungu  ila yametoka kwa daktari. Nilinunua dawa hapa Kenya. Sijafika bei ya daktari lakini mwezi Novemba nitaenda kufanyiwa upasuaji," Manzi wa Kibera alisema akiwa kwenye mahojiana na Mpasho.

Manzi wa Kibera alifichua kwamba hapo awali dawa alizokuwa akitumia zilifanya upande mmoja wa makalio yake kuwa mkubwa zaidi kuliko ule mwingine.

"Niling'ang'ana. Nikafanya kazi na nikafanya zitoshane.." Alisema huku akionyesha umbo wa makalio yake wa kumezewa mate.

Mwanasoshalaiti huyo alisema alikuwa anajifungia kwa nyumba sana wakati umbo wa makalio yake haukuwa sawa kutokana na athari za dawa.

Alifichua kuwa majirani wake walikuwa wanamkejeli kutokana na hali iliyokuwa imempata ndiposa alihofia kutoka nje.

"Sikuwa naenda mbali. Mbali sana ningeenda ni kwa mtu wa kuuza maharagwe juu napenda kuyala na chapati asubuhi. Nikishanunua nilikuwa narudi kwa nyumba na kutotoka tena. Sikuwa natoka kwa kuwa nikitoka majirani walikuwa wananikejeli ndiposa nikaacha. Nilisema sitatoka tena," Alisema.

Alifichua kuwa kuna mwanadada ambaye alimchanua kuhusu dawa ambayo angetumia ili kurekebisha hali hiyo.

Mwanasoshalaiti huyo alipata umaarufu mwaka jana kutokana na kipindi cha mchekeshaji Eric Omondi 'Wife Material'.