'Alikuwa atumbuize kwa saa 1 na dakika 30,' Mkurugenzi wa Klabu aliyesababisa kukamatwa kwa Harmonie azungumza

Muhtasari
  • Mkurugenzi huyo alisema kuwa wateja wake katika klabu hiyo hawakupata huduma walizotarajia
Mkurugenzi mkuu wa Konde Gang, Harmonize
Mkurugenzi mkuu wa Konde Gang, Harmonize
Image: instagram

 Mkurugenzi wa klabu ya Nairobi sasa anadai mwimbaji wa Tanzania Harmonize na timu yake warudishe pesa ambazo wateja wake walilipa kwa ajili ya tamasha yake Jumamosi usiku.

Akizungumza katika mahojiano na runinga ya Citizen, mkurugenzi wa klabu hiyo Joe Barsil alidai kuwa Harmonize alionekana jukwaani kwa chini ya dakika moja na kuondoka.

"Alipaswa hata kusalia katika klabu lakini malalamiko yangu makubwa ni njama ya timu nzima kulaghai. Maana nililipa pesa na hatukuwahi kupokea huduma," Barsil aliongeza.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa wateja wake katika klabu hiyo hawakupata huduma walizotarajia.

Barsil alithibitisha kwamba kandarasi hiyo inafafanua kwamba msanii anafaa kuonekana kwa angalau saa moja na nusu, kumaanisha hakuna mwonekano wa kiufundi unaoruhusiwa kama Eric Omondi alikuwa amesema kuhusu tamasha hilo.

Omondi na promota fulani, pia wamehusishwa na suala hilo.

Msanii wa Bongo Fleva nchini Tanzania amekamatwa na anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kileleshwa kwa madai ya kuruka muda wa kuonekana jukwaani katika Vilabu mbalimbali vya Nairobi.

Barsil aliendelea kusema kuwa jumla ya gharama ya klabu iliyoanzishwa na uchezaji wa Harmonize uligharimu karibu Sh1.45 milion

 

Mkurugenzi wa klabu aliyesababisha kukamtwa kwa Harmonize adai kurejeshewa pesa