Mike Sonko azungumza baada ya Harmonize kukamatwa

Muhtasari
  • Mike Sonko azungumza baada ya Harmonize kukamatwa

Mwimbaji wa Tanzania Harmonize alikamatwa mapema leo na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Kileleshwa kwa madai ya kukosa kufika katika vilabu kadhaa jijini Nairobi licha ya kupokea pesa kwa ajili yake.

Kulingana na ripoti, nyota huyo wa Bongo alishindwa kuonekana katika mojawapo ya makampuni yanayomilikiwa na aliyekuwa Gavana wa Kaunti ya Nairobi Mike Sonko licha ya kupokea Ksh3 milioni za malipo.

Sonko sasa amejitokeza na kuzungumia suala hilo huku akisema kwamba kutoelewana kidogo kati ya waandalizi kulisababisha mtafaruku huu.

"Aliitwa tu ili kuangazia kushindwa kutumbuiza. Kulikuwa na hitilafu ya mawasiliano na masuala madogo ambayo yalisababisha kutoelewana huku," gavana huyo wa zamani alisema.

Pia alisema kwamba Harmonize hakukosa kutumbuiza katika klabu yake huko Mombasa lakini anatazamiwa kutumbuiza leo kama rafiki na sio biashara.

Harmonize pia  anadaiwa kuwaacha washereheshaji wakiwa wamekata tamaa baada ya kutumbuiza kwa chini ya dakika tano.

Mcheshi Eric Omondi hapo awali alimtetea mwimbaji huyo kwamba kulikuwa na kutoelewana kutoka kwa mashabiki kuhusu kile ambacho Harmonize alitarajiwa kufanya katika klabu hiyo.

Omondi alisema kuwa Harmonize hakulazimika kuwatumbuiza washereheshaji usiku huo.

Dakika chache zilizopita Eric amepakia video huku akidai kwamba Harmonize amempiga ngumi baada ya kuenda kumtembelea msanii huyo kwenye kituo cha polisi.