Utazaa lini?-Shabiki amuuliza Anerlisa Muigai huku akimjibu haya

Muhtasari
  • Mwaka huu na katika mwaka mmoja uliopita tumewaona watu mashuhuri wakitangaza kubarikiwa na watoto
Anerlisa Muigai
Image: Anerlisa Muigai/INSTAGRAM

Mjasirimali Anerlisa Muigai, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amepokea maswali kadhaa kutoka kwa mashabiki huku mmoja wa mashabiki wake akimuuliza atajifungua lini.

Mwaka huu na katika mwaka mmoja uliopita tumewaona watu mashuhuri wakitangaza kubarikiwa na watoto.

Kulingana na shabiki huyo Anerisa alikuwa anazeeka na alipaswa kuwa na mtoto.

Mjasirimali huyo alivuma sana mitandaoni baada ya kufunga ndoa na msanii kutoka Tanzania Ben Pol, na baada ya muda mfupi wakatalikiana.

Anerlisa anaonekana kuendelea na masiha yake hata baada ya kurejea nchini na kuanza biashara, hivi majuzi Anerlisa alimtambulisha mpenzi wake wa sasa.

"Unapanga kupata watoto lini, unazeeka,?Shabiki aliuliza.

Kwa upande mwingine Anerlisa alimwambia shabiki huyo kwamba hajui atampata mtoto au watoto lini.

"Ata sijui," Alijibu Anerlisa.