"Katika maisha mengine bado ningekuchagua wewe," Kambua amsherehekea dadake

Becky Muikai anatimiza miaka 40.

Muhtasari

•Kambua ametambua ujasiri na upendo mkubwa ambao dada yake ameonyesha katika miaka mingi ambayo wamekuwa pamoja.

•Kambua na Muikai ni watoto wa marehemu Professor Manundu ambaye alikuwa daktari maarufu wa miti shamba.

Kambua na dadake Becky Muikia
Kambua na dadake Becky Muikia
Image: INSTAGRAM// BECKY MUIKIA

Dada mkubwa wa mwimbaji wa nyimbo za injili Kambua Manundu, Becky Muikai anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Kambua amechukua fursa hiyo kumsherehekea dadake na kumtakia kheri njema za siku ya kuzaliwa anapotimiza miaka 40.

"Mei 10, miongo 4 iliyopita msichana mzuri alizaliwa. Dada yangu mwenyewe! Mtoa Pepe, papai moto faya! My ride or die @beckymuikia!! Katika maisha mengine, bado ningekuchagua wewe dada yangu, mama wa watoto wangu," Kambua amemwandikia dadake kupitia Instagram.

Kambua ametambua ujasiri na upendo mkubwa ambao dada yake ameonyesha katika miaka mingi ambayo wamekuwa pamoja.

Isitoshe amemhakikishia Muikai kuhusu upendo wake mkubwa kwake na kumtakia mema anapofungua ukurasa mpya wa maisha yake.

"Tumevumilia misimu ya maisha pamoja na wewe, Becky umebaki kuwa thabiti. Ninaona jinsi unavyowapenda na kuwainua wengine. Msimu huu mpya uwe msimu wako wa kupendwa na kuinuliwa! Ah! Ikiwa hivi ndivyo ghorofa ya 4 inavyoonekana, ninaikimbilia. Wewe ni mrembo sana dada yangu! almaaufu Wanjiku almaarufu Bex almaarufu Rebecca (nani huyo)?😅 Nakupenda! Nakupenda! Mungu akulinde! Kheri za siku ya kuzaliwa!" Kambua ameandika.

Kambua na Muikai ni watoto wa marehemu Professor Manundu ambaye alikuwa daktari maarufu wa miti shamba.

Proffesor Manundu alikuwa na kipindi chake katika NTV ambapo alikuwa anatoa ushauri. Alifariki mwaka wa 2014.