Mimi nishawahi tuma 310 na nikagusa TV ndio nipone-Nyce Wanjeri afichua

Muhtasari
  • Zaidi ya yote alisema kwamba alituma pesa hizo na kugusa runinga yake
Nyce Njeri
Nyce Njeri

Mwigizaji Nyce Wanjeri almaarufu kama Shiro, alifahamika sana kupitia kwa bidii ya kazi yake kwenye sekta ya burudani.

Ni miongoni mwa waigizaji ambao wamejikakamua katika kazi yao, na kujiinua kimaisha, kutoka maisha ya uchochole hadi maisha ya utajiri.

Karne hii ya sasa kuna baadhi ya wahubiri ambao watashauri washiriki au watazamaji na wasikilizaji wao watume pesa ili waweze kupokea miujiza na uponyaji.

Wengi wameonekana kuwaamini wahubiri hao kwa sababu ya miujiza wanayofanya, huku baadhi ya Wakenya wakiwakejeli wahubiri kama hao.

Nyce kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram afunguka jinsi amewahi kuwa mwathiriwa wa kutuma pesa ili apone.

Zaidi ya yote alisema kwamba alituma pesa hizo na kugusa runinga yake.

"Usinione hivi hata Mimi nishawahi tuma 310 na nikagusa TV ndio nipone.I hope you will have a great day kuliko Jana," Aliandika Nyce.

Ni ujumbe ambao uliwafanya mashabiki kutoa maoni tofauti kuhusu tabia hiyo ya wahubiri.

Je umewahi tuma pesa ili uweze kupata miujiza na ulituma kiwango cha pesa ngapi?