Diamond atangaza mpango wa kununua ndege huku akifichua gharama kubwa ya gari lake

Muhtasari

• Diamond alifichua kuhusu mpango wake wakati akimtakia meneja wake El-Jefe Mendez heri za siku ya kuzaliwa.

•Picha zile zilionyesha kuwa gari hilo lilimgharimu Diamond pesa za Kiarabu AED 2, 250, 000 . (Ksh 71,200, 000/ Tsh 1.4B).

Diamond Platnumz na meneja wake EL-Jeffe Mendez
Diamond Platnumz na meneja wake EL-Jeffe Mendez
Image: INSTAGRAM// SALLAM SK

Nyota wa Bongo Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz ametangaza kuwa atakuwa mmiliki mpya wa ndege la kibinafi kifikia mwisho wa mwaka huu.

Diamond alifichua kuhusu mpango wake wakati akimtakia meneja wake El-Jefe Mendez heri za siku ya kuzaliwa.

Alihusisha mafanikio yake yote kwa usimamizi wake huku akiutaja  kuwa usimamizi bora zaidi duniani.

"Tulinunua 2021 Rolls Royce Black Bedge Zero Kilometre mwaka jana, na tunanunua ndege ya kibinafsi mwaka huu!! hiyo ndio tafsiri ya kuwa na usimamizi bora!! Ni Siku ya Kuzaliwa ya meneja wangu Sallam Sk," Diamond aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe wake na picha ya Sallam akiongoza shughuli ya ununuzi wa Roll Royce yake iliyofanyika mwezi Juni mwaka jana.

Picha zile zilionyesha kuwa gari hilo lilimgharimu Diamond pesa za Kiarabu AED 2, 250, 000 . (Ksh 71,200, 000/ Tsh 1.4B).

Tangazo la Diamond linathibitisha kauli ya mwandani wake Baba Levo ambaye siku chache zilizopita alidokeza kuhusu mpango huo.

"Nasema hivi! Ikifika mwezi wa kumi kama Diamond hajanunua ndege niuawe," Baba Levo aliandika kwenye Instagram.

Haya yanajiri huku hasidi wake Diamond, Harmonize akitangaza mpango wa kujitosa kwenye biashara ya sigara.

Harmonize ametuma ombi kwa mabwenyenye wa Tanzania kushirikiana naye kuanzisha kampuni ya kutengeneza sigara.

"Nataka mtu ambaye atawekeza vizuri. Tufanye hili pamoja. Hakuna haja ya kufanya hili pekee yangu. Nahitaji ushirikiano mkubwa. Kila mtu anajua kiasi gani mtaa unasubiri hii kitu kwa hamu," Harmonize alitangaza siku ya Jumatano.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide amefichua kuwa bidhaa yake itatambulika kama sigara ya Tembo.