'Wakenya ni washamba,'Huddah Monroe awashambulia wakenya waliokejeli dawa zake

Muhtasari
  • Huddah alisema bidhaa hiyo imekuwa sokoni kwa miaka kadhaa na ni kitu halali
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Huddah Monroe

Mmoja wa wanawake mashuhuri na mjasiriamali wa Kenya Huddah Monroe, amekuja na biashara mpya nchini Kenya na kimsingi inakusudiwa kuwasaidia wanawake au wanandoa kwa ujumla ili waweze kufurahia haki zao za ndoa.

Bidhaa hiyo ni kwa ajili ya kubana sehemu za uzazi wa mwanamke na angalau kumfanya mwanamume ajisikie vizuri anaposoma katiba.

Hata hivyo kumekuwa na hisia hasi kutoka kwa Wakenya, kwa sababu hili ni jambo jipya katika jamii yetu na pengine kwa baadhi ya tamaduni ni kinyume cha sheria.

Huddah Monroe ambaye anajishughulisha na uuzaji wa bidhaa hiyo, alijibu maoni hayo hasi kwa kusema baadhi ya Wakenya bado wana mawazo ya kutojua kusoma na kuandika na hii imewafanya kubaki nyuma.

Huddah alisema bidhaa hiyo imekuwa sokoni kwa miaka kadhaa na ni kitu halali.

"Watanzania na baadhi ya nchi za Afrika zinafahamu kuhusu bidhaa hii, ushamba ya Wakenya wengi na kujidai wanajua yote hamtaruhusiwa kuendelea maishani 

Kaa hapo na kamati yenu yaa roho chafu, unashangaa kwa nini wanaume hawakufanyii mambo hata kununulia chips mwitu kwa sababu hakuna motisha," Aliandika HUddah.