'Mke wangu ni mrembo kumshinda hawezi nipata,'Omanyala amjibu Huddah Monroe

Muhtasari
  • Hii ni baada ya kukiri kwamba wanaume waafrika hawajui kupenda au kudekeza wapenzi wao
  • Huku mwanariadha huyo akizungumza kuhudu jambo hilo amesema kwamba hana haja na mwanasosholaiti huyo
Ferdinand Omanyala
Ferdinand Omanyala
Image: HISANI

Siku chache ziliopita HUddah Monroe aliomba kuunganishwa na mwanariadha maarufu nchini Omanyala.

Hii ni baada ya kukiri kwamba wanaume waafrika hawajui kupenda au kudekeza wapenzi wao.

Huku mwanariadha huyo akizungumza kuhudu jambo hilo amesema kwamba hana haja na mwanasosholaiti huyo.

Zaidi ya yote Omnayala amekiri mkewe ni mrembo kumliko Huddah.

Katika mahojiano ya simu , Omanyala alizungumzia pendekezo hilo. Alicheka swali juu yake kukutana na Huddah na kuwa marafiki.

Kisha akasema, "Shetani Ashindwe! Huyo Hata Akituma Nini Bana Hawezi Nipata. Kitu Anaweza Pata Lay Nina. Simtaki, Nishafunga Hiyo Safari.

Omanyala akijibu swali la kuwa rafiki yake HUddah alisema kuwa;

"Hiyo itaniweka tu katika matatizo kwa sababu ndivyo inavyoanza na kisha inakua ndani ya kitu kingine. Katika ngazi mimi niko, kuna mambo unayohitaji kuepuka."

Alielezeakuwa amepitia hayo na mashabiki wa kike. Na yote anayotaka ni kuepuka shida yoyote na wanawake.

"Sio tu Huddah, nitaondoka! Ikiwa ninaona mwanamke yeyote anakuja kwangu na nia hizo zinazofanana, ninaondoka. Ninaondoa haraka kama kipchoge, haraka sana. Mimi ni mwaminifu sana kwa mke wangu."