Chipukeezy asema yuko single afichua aliachana na mpenzi wake

Muhtasari
  • Chipukeezy asema yuko single afichua aliachana na mpenzi wake
Chipukeezy
Image: Hisani

Hatimaye Chipukeezy amejitokeza wazi kufichua kwanini hashiriki tena maisha yake ya mapenzi kwenye mitandao ya kijamii na pia kwa nini hajaonekana akiwa na mpenzi wake anayefahamika sana Kibanja.

Akizungumza katika mahojiano n, Chipukeezy alisema kuwa uchumba na mahusiano ni mambo nyeti sana kuongelewa hadharani kwa sababu mambo yanazidi kubadilika, na kuna uwezekano watu wapenzi leo wanaweza kuachana kesho.

Chipukeezy aliweka wazi kwa kusema kuwa yeye yuko single na kwa sasa anafanya mahojiano kwa kukutana na marafiki zake wa jinsia nyingine na kujaribu kuona nani anawea kuwa mke mwema.

Alisema kuwa hatashiriki tena uhusiano wake kwenye mitandao ya kijamii, sasa ameelewa kwa nini uhusiano wa kibinafsi ni muhimu sana.

Alisema kuwa ana matumaini kuwa mwaka huu atapata mtu na kuoa faragha.

Alifichua kuwa yeye na Kartelo wamewahi kushirikiana katika mambo tofauti, sio ya kikazi tu bali pia ya kimaisha.

Chipukeezy alisema familia yake inampenda sana mfanyikazi mwenza huyo wake wa zamani kwa kuwa amewahi kusimama nao katika nyakati ngumu.

"Babu yangu alipoaga, Kartelo ndiye msanii pekee ambaye alihudhuria mazishi yake. Alikuja akakaa nasi, kila mtu katika familia yangu wanampenda Kartelo. Wanamuona kama ndugu. Kulingana nai, hatuwezi kukosana na Kartelo, Kartelo ni rafiki yangu. Ni mtu ambaye licha ya tofauti tunazoweza kuwa nazo tutabaki kuwa familia. Sisi ni familia kubwa," Alisema.