Aibu!Black Cinderella awakemea wanawake wanaowatambulisha wasichana wadogo kwenye ukahaba

Muhtasari
  • Black Cinderella awakemea wanawake wanaowatambulisha wasichana wadogo kwenye ukahaba
Muigizaji wa Nairobi Diaries Black Cinderella
Muigizaji wa Nairobi Diaries Black Cinderella
Image: Instagram

Nyote mnafahamu Black Cinderella ni nani na amekuwa akivuma kwenye mitandao hii ya kijamii kwa hisani ya pambano lake na mfanyakazi mwenzake Bridget Achieng.

Wawili hao wamekuwa wakitamba mtandaoni wakiitana majina mabaya na inaonekana wakati fulani Black Cinderella alidai kuwa hatawahi kuwa marafiki na Bridget Achieng kwa vile yeye ni adui wa watu.

Leo, Black Cinderella aliamka na habari fulani kwa mashabiki wake waaminifu kwenye Instagram na hii ilikuwa baada ya kutolewa kwa takwimu zilizodai kuwa wasichana 98 wanaambukizwa ukimwi kila siku.

Black Cinderella alihusisha hayo na uasherati na alisema kuwa wanawake hao ndio wanaowatambulisha wasichana wadogo kwenye maisha hayo na hatimaye kuambukizwa ugonjwa huo.

"Makahaba ulaani ukahaa wa mchana hadi kwenye wanaishi awpendi wwakionekana wakiend kazi, wewe na ujinga wako unakuja mitanddaoni na kutangaza kwamba unajiuza

Sababu umechanganyikiwa,ulikubai biashara hiyo kwa sababu ilikuwa inavuma bila kujua nini unachofanya kama unajua unapata pesa nzuri mbona umefanya ukahaba kwa zaidi ya miaka miwili

Pole kama una miaka 20,22,au 24 na tayari wewe ni maarufu katika biashara hiyo, aibu kwako,baadhi hamna sababu ya kuwa kwenye mitaa mnafuata kile kimevuma mna familia nzuri,ni ujinga tu mnafanya aibu kwenu aibu," Aliandika.

Black Cinderella alisema kweli kuwa kama kielelezo, ikiwa unatumia jukwaa lako kuonyesha jinsi unavyoishi maisha ya anasa na bado chanzo chako cha mapato ni kulala nje na wanaume wa kubahatisha wewe' kuathiri tena wasichana wadogo kwa njia mbaya.

Alikemea ukahaba akisema watu wafanye kazi hiyo ya chinichini bila kuwaathiri vibaya wasichana wadogo kwa sababu kwa sasa wasichana wameingiliwa ubongo na kuuza miili yao na hivyo ndivyo wanavyoishia kupata virusi vya ukimwi.

"Ujumbe wangu kwa wakenya wacheni kuwapa watu ovyo jina la umaarufu, kwani watu hawa ni mfano mwema kwa watoto wetu

Skiza kwa makini unaweza laani vikali ujinga au ukubali, lakini matokeo ya baadae yatategemea,tuna kizazi ambacho kinakuja baada yetu, lakini kwa bahati mbaya wanafariki wakiwa na miaka 25, ni jukumu letu kuwa mfano mwema kwa watoto hawa tuna ndugu na dada unaweza taka ndugu yao wa miaka aishi na virusi vya ukimwi."