Mfanyikazi wa Jalango amtaka Bien amuombe msamaha kwa kumtumia katika meme

Muhtasari
  • Litiema anadai kuombwa radhi kutokana na chapisho hilo alisema pia anastahili kupata kitu kwa sababu ya matumizi ya picha hiyo

Mfanyakazi wa mcheshi Jalango, Morrison Litiema amemlalamikia mshiriki wa Sauti Sol Bien Aime-Baraza kuhusu utumizi usioidhinishwa wa picha yake.

Bien alichapisha mtandaoni akiwa na picha ya Litiema ambaye alionekana akiwa amelala kitandani katika eneo ambalo lilionekana kuwa ni eneo dogo la watu wa kipato cha chini na kuweka maandishi ya kejeli,

"I am unsubscribing Sauti Sol illing in the crib".

Litiema alisema matumizi ya picha hiyo yalisababisha mateso ya kihisia kwani inafufua kumbukumbu za sehemu ambayo hangependa kurudi tena.

Mwanamume huyo aliyekasirishwa aliongeza kuwa picha hiyo ilisababisha shutuma kali kutoka kwa watu waliomshtumu kwa kutoshabikia muziki wa humu nchini ilhali hakuwa amejiondoa kwenye chaneli yoyote ya kijamii ya msanii yeyote wa Kenya.

“Kwa kaka yangu mpendwa Bien Aime Soul haikuwa sawa kutumia taswira yangu bila idhini yangu. Picha inayotumika imenifanya niteseke kihisia kwani ilinikumbusha sehemu ambayo sikuwahi kutamani kurudi tena

Nimepokea shutuma hasi kutoka kwa watu tofauti wanaodai kuwa siungi mkono wasanii wa ndani, ifahamike kwamba hawajawahi kujiondoa au kuacha kufuata akaunti yako ya YouTube au mitandao ya kijamii. Kwa hivyo, naomba msamaha kwa tukio lililotokea," aliandika. 

Litiema anadai kuombwa radhi kutokana na chapisho hilo alisema pia anastahili kupata kitu kwa sababu ya matumizi ya picha hiyo.