"Pepo zake ni nyingi!" Ringtone azungumzia tukio la Omosh kuanguka akiombewa na Pastor Kanyari

Muhtasari

•Omosh alisema pepo nyingi zilizokuwa zimeshambulia Omosh ziliwezwa na nguvu ya maombi na kusababisha muigizaji huyo kuanguka chini.

•Siku ya Jumapili Omosh alihudhuria ibada katika kanisa la Kanyari na mhubiri huyo akajitolea kumfanyia maombi.

Image: INSTAGRAM// RINGTONE APOKO

Mwimbaji wa nyimbo za injili Ringtone Apoko amesema wingi wa pepo ndio uliosababisha muigizaji Omosh kuanguka wakati alipokuwa akiombewa na mhubiri Victor Kanyari siku ya Jumapili.

Akiwa kwenye mahojiano na Nicholas Kioko, Omosh alisema pepo nyingi zilizokuwa zimeshambulia Omosh ziliwezwa na nguvu ya maombi na kusababisha muigizaji huyo kuanguka chini.

"Pale kuna shida kidogo. Sitaki kumuingilia Kanyari sana na pia sitaki kumuingilia Omosh sana . Lakini naona mapepo za Omosh zilikuwa zimelewa na ni nyingi ndio maana zikaanguka ata bila kupigwa na nguvu nyingi," Ringtone alisema.

Mwanamuziki huyo aliyezingirwa na utata mwingi alisema hana uhakika kuhusu uhalisi wa kipindi hicho cha maombi kati ya Omosh na Kanyari.

Hata hivyo alisema kuna uwezekano mkubwa tukio la muigizaji huyo kuanguka sio maigizo kwa kuwa nguvu za jina la Yesu zinaweza kufanya mtu kuanguka.

"Huenda ikawa Kanyari ni mkora, inaweza kuwa walikuwa wamepanga na Omosh. Lakini wakitaja jina la Yesu, hilo jina lina nguvu sana. Unaweza kuanguka ata kama ulikuwa umepanga," Alisema Ringtone.

Katika kipindi cha takriban siku mbili ambazo zimepita Omosh amekuwa gumzo tena mitandaoni baada ya video yake akianguka wakati akiombewa na mhubiri mashuhuri Victor Kanyari kusambaa.

Jumapili muigizaji huyo alihudhuria ibada katika kanisa la Kanyari na mhubiri huyo akajitolea kumfanyia maombi. Omosh pia alipokea vyakula kochokocho kutoka kwa mhubiri huyo.

"Nasikia Mungu akiniambia nikupandie mbegu. Nakubariki na pesa za tambiko. Nitakubariki na vitu zangu za kukula ziko hapa ofisini na pia nikubariki na elfu saba. Wakati huo mwingine wewe ndio utakuja kutuombea," Kanyari alisema kabla ya kumfanyia muigizaji huyo maombi.

Baada ya kumkabidhi bidhaa hizo Kanyari aliwekelea mkono wake kwenye utosi wa Omosh na kuanzisha maombi ambayo yaliishia kwa mwigizaji kuanguka chini kwa mgongo.