'Sio kila mwanamume yuko kwenye DM yako anataka kulala na wewe- Willy Paul kwa wanawake

Muhtasari
  • Ushauri wa Willy Paul kwa wanawake ulio zua hisia mtandaoni
Willy paul
Willy paul
Image: hisani

Kwa mara nyingine tena mwanamuziki wa Kenya na afisa Mkuu Mtendaji wa Saldido international entertainment Willy Paul amejipata akiwa upande mbaya wa mashabiki wake baada ya chapisho lake la hivi punde.

Mwimbaji huyo mnamo Mei 24, 2022, alishiriki kipande cha video kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram akiwashauri wanawake kwamba sio wanaume wote wanaotaka kulala nao.

Akiongeza kuwa wakati mwingine wanaume wanataka tu kujumuika nao na sio zaidi.

"Haya wanawake, mwanaume alipokutumia DM haimaanishi kuwa anataka kulala na nyinyi. Wengine tunapendeza na tunataka tu kujumuika na nyinyi."

Alisema zaidi kwamba wakati mwingine wanaume wanataka tu kujua jinsi wanavyoendelea.

"Tunataka kujua zaidi kuhusu wewe kama, nini kinakusumbua, kinachokusumbua, unajua! Kwa hivyo tafadhali pata hilo."

Hata hivyo, inaonekana hisia zake hazikuchukuliwa kirahisi na baadhi ya wanamitandao ambao walihisi kwamba hawako tayari kushiriki matatizo yao na wageni.