'Nitarudi na ubaya,'Vera Sidika atoa sababu ya kutokuwa Instagram kwa muda

Muhtasari
  • Vera Sidika atoa sababu ya kutokuwa Instagram kwa muda
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti maarufu nchini Vera Sidika kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ametoa sababu  ya kutokuwa kwenye mitandao hiyo kwa muda sasa.

Baada ya Vera kujifungua alikuwa anapakia picha za mwanawe, huku wengi wakimlimbikizia sifa mwanawe kwa urembo wa kipekee.

Vera Sidika alipata ujauzito mwishoni mwa 2020 na kujifungua 2021 kwa mtoto mzuri sana wa kike anayeitwa Asia.

Tangu wakati huo Vera Sidika aliacha kuchapisha picha chafu sana kwenye Instagram kama hapo awali alipokuwa akishiriki picha za wazi kwenye Instagram.

Nadhani hiyo ndiyo sababu watu wengine wanadhani Instagram inachosha.

Amekuwa kimya na hatujawahi kumuona akijihusisha na vita vya mtandaoni au kashfa kama hapo awali.

Hata hivyo Vera Sidika amesema kuwa anakaribia kurejea tena.

"@breeder_lw 🎶IG ilibooo after Vera Apate Mimba🎶 😂😂😂😂 manze I’ve been on leave but narudi na ubayaaaa. The IG streets zinabooo kweli. But zitachangamka very soon. Clock’s ticking ⏰ Tighten your seat belts!!!! Very Soon the Queen is baaaaack!!!!," Aliandika Vera.