Rick Ross athibitisha anamchumbia Hamisa Mobetto

Muhtasari
  • Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza wakiwa Dubai, Hamisa alipokuwa mapumzikoni lakini walikuwa marafiki kwa muda mrefu
Hamisa Mobetto na Rick Ross
Hamisa Mobetto na Rick Ross
Image: INSTAGRAM

Rapa na mtayarishaji wa rekodi kutoka Marekani, William Leonard Roberts II, maarufu kwa jina la Rick Ross amethibitisha kuwa ana uhusiano na mfanyabiashara, mwigizaji, mwimbaji na mshawishi wa chapa Tanzania Hamisa Mobetto.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 46 alithibitisha uhusiano wao kwenye kipindi cha hivi karibuni cha instagram na Hamisa Mobetto.

“Wanataka kujua kama tunachumbiana au la na wanataka ujibu,” Hamisa alisema na Rick Ross akajibu

“Ndiyo ni wangu, ni wangu.” Hamisa alitabasamu tu lakini hakusema kama walikuwa wanachumbiana kweli au la.

Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza wakiwa Dubai, Hamisa alipokuwa mapumzikoni lakini walikuwa marafiki kwa muda mrefu.

Huko Dubai, Rick Ross alishindwa kujizuia kumwonyesha mama huyo wa watoto 2 kwa sababu ya urembo wake na walionekana wakistareheshana mara nyingi, tetesi za uchumba ambazo hazijathibitishwa.