'Furaha ndio unakosa,'Wema Sepetu amrushia vijembe mwanablogu Mange

Muhtasari
  • Wema amemuonya mwanablogu huyo na kumwambia anapaswa kumkoma na wakati huu anamaanisha achosema
wema 5 (1)
wema 5 (1)
Image: HISANI

Mwigizaji wa filamu za Bongo Bi. Wema Sepetu amemjibu mwandishi wa habari mitandaoni Mange Kimambi baada yake kuchapisha madai kwamba Wema anatumia hela kununua wafuasi kwenye mtandao wa Instagram.

Wema ambaye amemrejelea Mange kama “Manunu mkubwa” Manunu likiwa jina la mbwa wake, anasema hakuna siku amewahi kuhangaika kutafuta wafuasi kwenye mitandao ya kijamii.

Wema amemuonya mwanablogu huyo na kumwambia anapaswa kumkoma na wakati huu anamaanisha achosema.

Huku nikinukuu alichoandika wema, aliandika kuwa;

"Kwa hio ulikuwa unataka kusemaje labda nikuulize?..huna jipya bwana weee,shamba la wazungu hiloo...ila una kaulimbukeni flani pia nimegundua..kama wewe unababaika na wazungu sio kila mtu...mu mzima kiazi maisha yangu yanakuuma sana wee

Utaishi hayo hayo jitu zima ovyo,mbwa ni mbwa tu habadaliki..ebu nipishe mie huna jipya alafu usinichoshe ujue sitaki," Wema Aliandika.

Mange Kimambi ni mzaliwa wa Tanzania ambaye anaishi nchini Marekani na hivi maajuzi ameanzisha App yake ya mitandaoni ambayo anatumia kwa kuuza habari na uvumi pamoja na vipindi ingine kikiwemo kipindi cha mapishi na lishe.

Wema alimshauri Mange akatafute furaha kwani ndio anakosa maishani mwake.

"Furaha ndio kitu unakosa katafute,ushauri kutoka kwa ex wako mdogo,hunitishi bwana kituko cha taifa."