'Asante kwa kuwa nguzo yangu maishani,'Esther Musila amkumbuka marehemu mama yake

Muhtasari
  • Mkewe mssanii wa nyimbo za injili Guardian Angel,Esther Musila kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemkumbuka marehemu mama yake

Mkewe mssanii wa nyimbo za injili Guardian Angel,Esther Musila kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemkumbuka marehemu mama yake.

Musila alimpoteza mama yake miaa 6 iliyopita.

Kulingana na Musila mama yake alikuwa nguzo yake na alimfunza kuthamini kila siku ya maisha yake.

Huku akimkumbuka marehemu mama yake aliandika ujumbe huku akimsifia na kusema kuwa;

"Miaka 6 iliyopita, asubuhi kama hii, nilipokea simu kwamba mama yangu mpendwa amefariki dunia usingizini

Hii ilikuwa chini ya saa 12 baada ya mimi na kaka yangu Fred kwenda kwenye shags kwa wikendi. Ilikuwa siku ya giza zaidi katika maisha yetu. Bado sijui tulipataje nguvu ya kuendesha gari hadi Machakos, kwa kweli ilionekana kama ndoto na tungetoka nje

Ninaamini kabisa hadi leo kwamba Mwenyezi alilitatua kwa njia yake mwenyewe na alitaka tutumie saa za mwisho za maisha ya mama pamoja naye.

Mama, asante kwa kuwa nguzo yangu maishani. Ulinifundisha kuthamini kila siku ya MAISHA yangu na kuishi kana kwamba hakuna kesho. Nililelewa na mwanamke mwenye nguvu na najua huwa unanipa mgongo mama yangu.

Pumzika kwa Nguvu mama yangu kipenzi. Ninathamini MAISHA tuliyoshiriki pamoja."

Mama huyo allisema kwamba anatamani mama yake angeishi na kukutana na mumewe Guardian Angel.

"Mama, natamani ungeishi muda mrefu zaidi ili kukutana na mwanamume mzuri zaidi maishani mwangu sasa. Najua ungefurahi sana kuniona katika nafasi hii mpya na nakuwekea dau, tungekuwa tukiimba pamoja nyimbo uzipendazo.

Tunakukumbuka na kukupenda milele Mummy ❤❤❤."