Bien azungumzia alivyomsaidia Flaqo kupambana na msongo wa mawazo

Muhtasari

•Bien amekubali kuwa ni kweli alimsaidia mchekeshaji Flaqo wakati alikuwa anakumbwa na msongo wa mawazo.

•Mwanamuziki huyo ametoa wito kwa wasanii wengine kuchukua muda wa mapumziko ili kutuliza akili zao.

Bien na Flaqo
Bien na Flaqo
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki wa Sauti Sol Bien-Aime Baraza amekubali kuwa ni kweli alimsaidia mchekeshaji Flaqo wakati alikuwa anakumbwa na msongo wa mawazo.

Akiwa kwenya mahojiano na Plug TV, Bien alisema alijitolea kusaidia mchekeshaji huyo kama shabiki na ndugu yake mkubwa.

Bien alisema  alielewa hali ambayo Flaqo alikuwa anapitia kwa wakati huo. Amesema kuwa anafurahia kuona hatua ambazo mchekeshaji huyo amepiga baada ya mazungumzo yao.

"Vile alinipigia nilihisi ni jukumu langu kama ndugu yake mkubwa. Kwa ujumla mimi kama shabiki wa Flaqo ilibidi nihakikishe kuwa yuko sawa kwa sababu hatugudui yale ambayo Flaqo hufanya. Yeye ni kama Eddy Murphy, kucheza nafasi sita kwaweza kuchokesha sana. Namuelewa na nafurahia kuwa amerudi sawa," Bien alisema.

Mwanamuziki huyo ametoa wito kwa wasanii wengine kuchukua muda wa mapumziko ili kutuliza akili zao.

Siku chache zilizopita Flaqo alijitokeza kufichua sababu kwa nini alikuwa amekosekana kwenye sanaa kwa kipindi kirefu.

Flaqo alisema alilazimika kupumzika kwa sababu ya matatizo ya afya ya akili huku akieleza  kuwa licha ya umaarufu mkubwa ambao alikuwa amejizolea hakuwa na furaha sana.

"Nakumbuka nilimaliza shoot, nalikuwa na hisia fulani, Bien anajua haya, nilimpogia Bien simu nikaanza kusema mambo hata hayana maana,alinipa namba ya simu ya mtaalamu, ilikuwa hisia fulani sijui niseme Bipolar au Depression, nimekuwa nikipigana na hayo kwa mwaka mmoja sasa," Flaqo alisema.

Mchekesahaji huyo alisema safari ya kupata afueni na kurejelea hali ya kawaida haijakuwa rahisi kwake.

Flaqo alifichua kuwa amekuwa akitembelea mtaalamu wa masuala ya kisaikolojia kwa kipindi cha  mwaka ambacho kimepita na kuweka wazi kuwa sasa yupo sawa.