Huwezi nunua amani ya akili mchague mpenzi wako vyema-Huddah Monroe kwa wanawake

Muhtasari
  • Kulingana na mwanasosholaiti huyo wanawake wanapaswa kuwachagua wapenzi wao vyema kwani hawawezi kununua amani ya akili
Huddah Monroe
Image: Facebook

Mwanasosholaiti Huddah Monroe kwa mara nyingine amewapa wafuuasi wake wa kike ushauri kuhusu uhusiano wa mapenzi.

Kulingana na mwanasosholaiti huyo wanawake wanapaswa kuwachagua wapenzi wao vyema kwani hawawezi kununua amani ya akili.

Pia amesema kwamba asilimia kubwa ya wanawake huenda wakajisahau wanapokuwa kwennye uhusiano wa kimapenzi na kukiri hujisahau akiwa na mpenzi wake.

"Wanawake ujihusisha na uhusiano wa kimapenzi na kujisahau,mimi nikiwa mmoja wao, napenda mapenzi nimekuwa daima kwe ye uhusiano, na huwa nasahau ulimwengu wote ninapokuwa na mpenzi wangu

Wakati mwingine ni mzuri, lakni chagua mpenzi anaye faa roho yako," Alizungumza Huddah.

Aidha amesema kwamba amani ya akili ni ya gharama ya juu zaidi.

"Ni vyema kupotea kwenye roho nzuri,amani ya akili ni ya gharama ya juu hamna kiasi cha pesa ambacho kinaweza nunua

Ukweli ni kuwa amani ya akili haiwezi nunuliwa,ndio maana unaona tajiri mkubwa akijitia kitanzi au mwanamke ambaye ammefanikiwa akiwa na msongo wa mawazo unashindwa kwa nini."