Akothee atengana na mpenzi wake Nelly Oaks

Muhtasari

•Akothee hata alifikia hatua ya kufuta picha zake zote na Oaks ambazo aliwahi kuchapisha hapo awali.  

Nelly Oaks na Akothee
Nelly Oaks na Akothee
Image: Instagram///AKOTHEE

Akothee na Nelly Oaks wameibua sintofahamu kuhusu mahusiano yao baada ya kuamua kutofuatana katika mitandao ya kijamii.

Isitoshe, mama huyo wa watoto watano alifikia hatua ya kufuta picha zake zote  na Oaks ambazo aliwahi kuchapisha hapo awali.  

Wapenzi hao ambao walikuwa wakimiminiana sifa  kemkem kwa takriban mwaka mmoja wanaonekana kuyazika mahusiano yao kwenye kaburi la sahau.

Wakenya wamepokea habari hizo kwa mchanganyiko wa mshangao na kutojali ikizingatiwa kuwa kweli hili ni jiji la Nairobi ambapo kutengana ni jambo la kawaida sawa na ufisadi.

 Wakati huo huo baadhi ya watu wengine wamehoji ikiwa ni kiki tu ambayo wawili hao wanatafuta, jambo ambalo hatuwezi kuthibitisha  hadi wawili hao wazungumze wenyewe.

(Utafsiri: Samuel Maina)