Haitawahi fanyika-Miss P asema haya kuhusu kufanya kazi tena na Willy Paul

Muhtasari
  • Wawili hao hata hivyo walitengana mwishoni mwa 2021, na hii ilikuwa baada ya mrembo huyo kumshutumu Pozze kwa mengi
Miss P na Willy Paul
Image: INSTAGRAM

Ni wazi kuwa waimbaji Willy Paul na Miss P siku moja hawataweka tofauti zao kando na kufanya kazi tena pamoja.

Hii ni kwa sababu hilo sasa halitatimia, na ni kweli mrembo huyo ndiye aliyehakikisha hilo kupitia kipindi cha hivi majuzi cha Maswali na Majibu ambacho alikuwa nacho na mashabiki wake kwenye hadithi zake za insta.

Alipoulizwa ikiwa wimbo mwingine na Pozee ulikuwa ukikaribia, jibu lake lilikuwa hapana.

Alifichua zaidi kwamba sababu kuu ya hii ni kwa sababu wote wawili walikuwa na kiburi sana kufanya kazi na mtu mwingine.

"KIbao kingine na Pozzee," Shabiki aliuliza.

"Kusubiri kumeisha, halitawahi fanyika kwa sababu sisi sote tuna kiburi," Alijibu Miss P.

Itakumbukwa kwamba Miss P aliwahi kusainiwa na lebo ya rekodi ya Willy Paul ya Saldido International, na wawili hao walichukua nchi kwa dhoruba kwa kuachia nyimbo maarufu kama 'Liar' na 'Fall In Love'.

Wawili hao hata hivyo walitengana mwishoni mwa 2021, na hii ilikuwa baada ya mrembo huyo kumshutumu Pozze kwa mengi jambo kuu likiwa ni unyanyasaji wa kijinsia.

Baada ya shutuma hizo, aliachana na lebo hiyo na sasa amesajiliwa chini ya Jabali Entertainment.