Kila mwanamke anastahili mwanamume anayemkubali-Nyota Ndogo asema

Muhtasari
  • Kulingana na Nyota Ndogo anafichua kuwa mume ni mkubwa na tofauti ya umri wa miaka ishirini
Nyota Ndogo na mumewe Henning Nielsen.
Nyota Ndogo na mumewe Henning Nielsen.
Image: INSTAGRAM// NYOTA NDOGO

Mwanaisha Abdalla anayejulikana kama Nyota Ndogo ni mwanamuziki maarufu wa Taarab mwenye Ushawishi nchini.

Kando na kuwa mwanamuziki, yeye pia ni mfanyabiashara na amekuwa akitumia mtandao kwa mbwembwe kutokana na kauli tata zinazohusu maisha yake ya uhusiano ambazo zimesambaa kila mara.

Nyota Ndogo ameolewa na Mholanzi Henning Nielsen na wanandoa hao wamekuwa wakionyesha mapenzi yao mtandaoni hivyo basi kuwavutia Wakenya wengi.

Kulingana na Nyota Ndogo, amesisitiza kuwa mume amekuwa mwaminifu kwake na amekuwa mshauri mzuri kwake na mshauri ambaye amemwezesha kupata mafanikio mbalimbali ya kibinafsi. katika maisha yake.

Kulingana na Nyota Ndogo anafichua kuwa mume ni mkubwa na tofauti ya umri wa miaka ishirini.

Nyota Ndogo amemsifu muewe huku akifichua kuwa amejifunza mambo mengi kutoka kwake.

"Tueke tu mzaa kando.kila mwanamke anastaili mwanamume anamkubali alivyo anae msapoti kwa kila jambo zuri anaempa ushauri na unapofanya kitu kisifaulu anakwambia jaribu tena.this man yani my husband ameliona jua mbele yangu kwa miaka ishirini kabla mimi kuzaliwa kwa kunavitu vingi najifunza kwake.hapa nipo na mume na baba pia.thank you my husband hennin.i love you..WATAONGEA MENGI LAKINI MUIMU SISI TUNAPENDA."