Jux amkubali Huddah zaidi ya aliyekuwa mpenzi wake Vanessa Mdee

Muhtasari

•Jux alikiri kuwa wote wawili ni wanadada warembo ila akadai Huddah anampiku Vanessa kwa kiwango ambacho hakuthibisha.

•Jux alichumbiana na Vanessa kwa takriban miaka sita ila mahusiano yao yakagonga mwamba mwaka wa 2019.

Image: INSTAGRAM// JUMA JUX

Staa wa Bongo Hip Hop Juma Jux alikuwa mgeni katika kipindi cha Big Sunday Live kwenye Wasafi TV siku ya Jumapili.

Katika kipindi hicho Jux alifunguka kuhusu mambo kadhaa yanayohusiana naye na watu ambao wamewahi kuwa wa karibu naye.

Mojawapo ya swali ambalo msanii huyo alitegwa nalo ni anamkubali nani zaidi kati ya mpenzi wake wa zamani Vanessa Mdee na mwaasoshalaiti Huddah Monroe ambaye anadaiwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi naye kwa sasa.

Jux alikiri kuwa wote wawili ni wanadada warembo ila akadai Huddah anampiku Vanessa kwa kiwango ambacho hakuthibisha.

"Kusema kweli, wasichana wote ni wazuri hapa (Vanessa na Huddah). Vanessa ni mrembo, Huddah ni mrembo pia. Pisi zote kali kwa sababu kila mmoja ni mzuri kwenye sekta yake. Kiukweli wamezidiana, kuna vitu navipenda kwa Huddah na kuna vitu navipenda kwa Vanessa. Lakini kwa ufupi nampa Huddah," Jux alisema.

Jux alichumbiana na Vanessa kwa takriban miaka sita ila mahusiano yao yakagonga mwamba mwaka wa 2019. Miezi kadhaa baadae Vanessa alijitosa kwenye mahusiano na muigizaji Rotimi kutoka Marekani ambaye tayari wana mtoto mmoja pamoja.

Siku za hivi majuzi kumekuwa na tetesi nyingi kuwa Jux anachumbiana na Huddah ambaye ni mwanasoshalaiti maarufu  kutoka Kenya.

Madai kuwa wawili hao wanachumbiana yalivuma zaidi baada yao kuonekana wakibusu hadharani mara kwa mara.

Hata hivyo wasanii hao wawili tayari wamejitokeza kueleza kuwa uhusiano wao ni wa kirafiki ila sio wa kimapenzi.

"Mimi nipo kwenye mahusiano na najua Huddah yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi. Kwahiyo swala la sisi wawili kuwa wapenzi halijitokezi. Lakini nitalijibu swali hili siku nyingine. Lolote linaweza kutokea." Jux alisema katika mahusiano ya hapo awali.

Pia kumekuwa na tetesi kuwa Jux alitemwa na mpenzi wake halisi hivi majuzi kufuatia uhusiano wake wa karibu na Huddah.