Pritty Vishy afunguka jinsi Stivo Simple Boy alivyomtongoza

Muhtasari

•Pritty Vishy alifichua kuwa Stivo alimkatia wakiwa nyumbani kwa nyanya yake katika mtaa wa Kibera.

• Stivo alisema walikubaliana na Vishy amalize masomo yake hadi shule ya upili ili waweze kufunga ndoa.

Image: INSTAGRAM// PRITTY VISHY

Pritty Vishy amefichua kuwa Stivo Simple Boy ndiye aliyechukua hatua ya kwanza katika kuchumbiana kwao.

Akiwa kwenye mahojiano na Oga Obinna, Vishy hata hivyo alieleza kuwa mwanamuziki huyo hakuweka juhudi nyingi katika kumtongoza.

"Aliniambia tupendane, tutakane. Nikamwambia chonjo. Kaende," Alisema.

Kipusa huyo mwenye umri wa miaka 20 alifichua kuwa Stivo alimkatia wakiwa nyumbani kwa nyanya yake katika mtaa wa Kibera.

Alieleza kuwa mwanamuziki huyo alikuwa anaenda kumtembelea kwa nyanyake baada ya kutofautiana na dada yake.

"Singeenda kwao kwa sababu hatukuwa tunaelewana na dada yake," Alisema.

Katika mahojiano ya awali Simple Boy aliweka wazi kuwa yeye ndiye aliyemkatia Pritty Vishy. Alisema walijuana wakati Vishy alikuwa katika darasa la nane.

 Stivo alisema walikubaliana na Vishy amalize masomo yake hadi shule ya upili ili waweze kufunga ndoa.

"Tulikutana kitambo akiwa darasa la nane. Nilimwambia akimaliza shule aende shule ya upili bado nitakuwa nimemsubiri," Stivo alisema.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa alimpenda sana kipusa huyo mwenye umri wa miaka 20 ila akakosa subira.

Alidai kuwa mpenzi huyo wake wa zamani hakuwa mwaminifu na aliwahi kutoka kimapenzi na wanaume zaidi ya 50 katika kipindi cha mahusiano yao.

"Mimi nilinyamazia tu. Nilikuwa nikimwambia  kama ananipenda cha kweli awachane na hayo mambo yake. Nilimwambia akuwe na mtu mmoja ili tufunge ndoa. Lakini haeleweki jameni," Alisema katika mahojiano na Obinna.

Vishy hata hivyo amepuuzilia mbali madai ya kutoka kimapenzi na wanaume wengine huku akieleza kuwa msanii huyo alikosa kumwamini.

Shida ya Stivo ata akiniona kwa barabara nikitembea na mjomba wangu jioni angekuja aniambie alisikia nilikuwa natembea na mwanaume. Nilishangaa kwani sifai kutembea na watu kwa sababu nachumbiana na yeye.Huyo ni mpenzi sumu," Vishy alisema.

 Alisema ikiwa Simple Boy alifahamu kuwa hakuwa mwaminifu basi angekatiza mahusiano yao.